Sunday, June 26, 2011

LEO DUNIANI

Mkuu wa majeshi ya Ujerumani ajiuzulu

Akitoa taarifa hiyo bungeni Waziri wa ulinzi wa Ujerumani, Karl-Theodor zu Guttenberg, alisema Bwana Schneiderhan ameomba mwenyewe kuacha kazi.

Kamanda Schneiderhan amechukuwa uamuzi huo kutokana na lawama kwamba wizara ya ulinzi ilizuwi kutoa maelezo kwa wananchi na kwa mwendesha mkuu wa mashtaka kuhusu raia waliouawa kwa shambulio la ndege liloamriwa kufanywa na jeshi la Ujerumani mwanzoni mwa mwezi Septemba nchini Afghanistan.Shambulio hilo lililengwa dhidi ya malori ya mafuta.

Hapo kabla, waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Guido Westerwelle, alishikilia kurefushwa muda wa kuyabakisha majeshi ya Ujerumani katika Afghanistan, na, wakati huo huo, akatangaza kwamba serikali itakuwa wazi na itasema ukweli juu ya shughuli za jeshi hilo.

Serekali itarefusha muda wa jeshi hilo kuweko Afghanistan kwa mwaka mmoja hadi mwisho wa mwaka 2010. Idadi ya wanajeshi hao 4,500 itabakia hivyo hivyo , bila ya kubadilika.

Lakini kwa mujibu wa Gazeti linalochapishwa mjini Cologne , Kölner Stadt-Anzeiger, wizara ya ulinzi inafikiria kuongeza idadi ya wanajeshi wa Ujerumani nchini Afghanistan kufikia 6,500.

Israel kusimamisha kwa muda ujenzi wa makazi


Israel imetangaza kuusitisha kwa muda wa miezi kumi ujenzi wa makazi ya Wayahudi katika eneo la Ukingo wa Magharibi.Kauli hizo zimetolewa na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliyefafanua kuwa hatua hiyo haitouathiri ujenzi wa majengo ya umma.Punde baada ya kukikamilisha kikao cha baraza la mawaziri,Waziri Mkuu Netanyahu aliyezungumza na waandishi wa habari aliwatolea wito Wapalestina kuyafufua mazungumzo ya kusaka amani ya mashariki ya kati.Marekani imefurahishwa na hatua hiyo ila WaPalestina wamekata kuuitikia wito huo.Kulingana na mpatanishi mkuu Saeb Erakat, wito huo hauna lolote jipya na Israel bado itaendelea na ujenzi wa makazi alfu 3 ambao ulishaanza.Mwanadiplomasia huyo aliongeza kuwa kwavile suala la hatma ya eneo la Jerusalem Mashariki halikutajwa,mazungumzo hayo ya kusaka amani hayatoanza tena.Mazungumzo hayo yamekwama kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja.

Baba Mtakatifu aongoza sherehe za krismasi.

Sherehe za kuadhimisha krismasi zimeanza duniani kote.

Baba mtakatifu Benedikt wa 16 ,kama desturi aliongoza sala jana usiku. Awali Papa alijitokeza dirishani kwenye uwanja wa mtakatifu Petro na kuwasha mshumaa kama ishara ya amani. Katika ujumbe wake baba mtakatifu ametoa wito juu ya kukomesha chuki na umwagaji damu katika mashariki ya kati.

Na Katika mji wa Bethlehem, kwenye ukingo wa magharibi, mamia ya watu walijipanga foleni ili kusali katika kanisa la uzawa wa Yesu Kristo ambapo kihistoria Bethlehem ndiyo mji ambako Yesu Kristo alizaliwa.

Hotuba ya Krismasi ya Papa

VATICAN

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Benedikti wa 16, ametoa wito kwa ulimwengu kuachana na vurugu na machafuko katika hotuba yake ya sikukuu ya Krismasi. Papa Benedict alitoa hotuba hiyo saa chache baada ya kuangushwa chini na mwanamke aliyeruka vizuizi vya usalama katika misa ya mkesha wa Krismasi. Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Susana Maiolo, ametajwa kuwa na historia ya matatizo ya akili na aliwahi pia kujaribu kumkaribia kiongozi huyo wa kidini mwaka uliopita lakini akazuiwa. Kiongozi huyo wa kidini, hata hivyo, alinyanyuka mara moja baada ya tukio hilo la kuanguka na kuonekana kuwa katika hali nzuri ya kiafya wakati akihutubia umati wa wafuasi waliokuwa wamekusanyika katika uwanja wa kanisa la St Peters.

Maaskofu wa Ireland wajiuzulu kutokana na kashfa ya ulawiti.

DUBLIN

Maaskofu wengine wawili wa kanisa Katoliki nchini Ireland wamesema kwamba watajiuzulu kufuatia kufichuka kwa kashfa kwamba dayosisi kuu ya Dublin imekuwa ikificha vitendo vya kulawiti vilivyokuwa vinafanywa na makasisi dhidi ya watoto. Maaskofu wasaidizi, Eamonn Walsh na Ray Field, wamesema wanatumai hatua yao ya kujiuzulu inaweza kusaidia kuleta amani na maridhiano ya Yesu Kristo kwa wahanga na watoto walionusirika na vitendo hivyo vya ulawiti. Ripoti iliyotayarishwa na serikali ya Ireland, imefichukua kuwa kanisa Katoliki limekuwa likificha vitendo hivyo vya kuwalawiti watoto wadogo kuanzia mwaka 1974 hadi mwaka 2004 pamoja na kuwalinda makasisi 170 waliokuwa wakiendesha vitendo hivyo wasichukuliwe hatua za kisheria.Tangu kutolewa kwa ripoti hiyo takriban mwezi mmoja uliopita, maaskofu wengine wawili, tayari wamejiuzulu.

Shambulizi katika ndege ya kuelekea Marekani.

WASHINGTON

Rais Barack Obama ameagiza kuchukuliwa hatua za ziada za kiusalama katika usafiri wa ndege, baada ya mtu mmoja kujaribu kulipua ndege moja ya shirika la Marekani iliyokuwa inaelekea Detroit kutoka mjini Amsterdam. Mtu huyo ambaye anasemekana ni raia wa Nigeria, alikuwa abiria ndani ya ndege hiyo, yenye chapa AIRBUS 330 iliyokuwa imewabeba abiria 278, alizidiwa nguvu na wenzake alipojaribu kuwasha fataki wakati ndege hiyo ilikuwa inatua katika uwanja wa ndege huko Detroit. Vyombo vya habari vya Marekani, vinaripoti kuwa mtu huyo amewaambia maafisa wa usalama kuwa alitoa fataki hizo na maagizo ya kuilipua ndege hiyo kutoka nchini Yemen. Rais Obama ambaye yuko likizoni huko Haiwaii anasemekana anafuatilia matukio, lakini hajabadili ratiba yake. Taarifa kutoka shirika la ndege la Northwest zinasema raia huyo wa Nigeria amekamatwa na abiria wengine walihojiwa kufuatia tukio hilo.

Kumbukumbu ya Tsunami miaka 5

ACEH, INDEONESIA

Raia wa jimbo la Aceh nchini Indonesia wametenga leo kuwa siku ya maombi, kuwakumbuka wahanga wa janga la Tsunami lililokumba bara Asia miaka mitano iliyopita. Kiasi cha watu elfu 200 waliuawa, na mabilioni ya mali kuteketezwa. Eneo la Aceh, huko Indonesia ndilo lililoathirika zaidi, kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililosababisha Tsunami Desemba tarehe 26 mwaka wa 2004. India, Sri Lanka na Thailand ambazo pia ziliathirika, zimetenga leo kuwa siku ya maombi kama kumbukumbu ya janga hilo. Hapa nchini Ujerumani, maombi yatafanyika katika kanisa moja mjini Dusseldorf.

Mashambulizi yatokea nchini Iraq.

BAGHDAD

Watu 18 wameuawa, nchini Iraq, katika mashambulizi mapya licha ya usalama kuimarishwa katika sikukuu ya Krismamasi, pamoja na sherehe za Ashura zinazofanyika katika jamii ya Washia nchini humo. Watu sita waliuawa, kufuatia mripuko wa bomu lililokuwa limetegwa barabarani, lilipolipuka wakati msafara wa Washia walipokuwa wanapita huko Sadr, Baghdad. Watatu kati ya waliouawa wanasemekana ni waalimu waliokuwa wakikusanya data, za taasisi ya kuhesabu watu nchini Iraq. Zaidi ya polisi elfu 46 na wanajeshi wamepelekwa katika miji ya Karbala na Najaf, kushika doria, leo katika sherehe za siku ya Ashura

Wimbo bora wa injili mwaka 2009

Nyimbo za injili zipatazo 30, zimeingizwa katika kinyang’anyiro za kutafuta wimbo bora wa mwaka 2009. Shindano hilo linaendeshwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1). Watazamaji wa TBC1 wanatakiwa kuchagua wimbo mmoja kati ya hizo, kisha kupiga kura kwa kuandika jina la wimbo na namba ya mhusika kwenda 15788. Kipindi cha shindano hilo kinarushwa majira ya saa 3:15 usiku kuanzia Desemba 25 mpaka 27. Mshindi wa atapatikana Desemba 27 mwaka huu.

Waimbaji waliokatika shindano hilo na namba zao za ushiriki kwenye mabano ni;

Neema Mwaipopo – Usijinyime raha (101)

Jenn Joel Makila - Mungu hana upendeleo (102)

Jennifer Mgendi – Jaribu langu (103)

AIC Chang’ombe – Mpinga Kristo (104)

Medrick Sanga - Mapambano (105)

Mwanga town Choir – Mwambie Yesu (106)

Ency Mwalukasa – Usilie (107)

AIC Mwadui – Haki (108)

Apostle Kyande – Selemala (109)

AIC Makongo – Kekundu (110)

Rose Mahenge – Mbinguni ndiko nyumbani (111)

Jenn Miso – Omoyo (112)

Solomon Mukubwa – Mfalme (113)

Upendo group – Jina lako li hai (114)

Rose Mhando – Jipange sawasawa (115)

Upendo group – Yesu yeye yule (116)

Flora Mbasha – Furaha yako (117)

Rose Mhando – Si salama (118)

Joseph Nyuki – Tegemeo langu (119)

Mt. Cecilia Arusha – Nimevunja mkataba na shetani (120)

Upendo group – Mungu wetu ni mwema (121)

Geraldine Odwaa – Upendo wa ajabu (122)

Upendo group – Amen haleluya (123)

Abiud Misholi – Tenda miujiza (124)

Christina Shusho – Unikumbuke (125)

Ado November – Amenitoa mbali (126)

Upendo Nkone – Haleluya usifiwe (127)

Mhubiri kwaya – Nani kama wewe (128)

Rose Mhando – Nibebe (129)

Bahati Bukuku – Waraka (130)

Piga kura sasa kwa wimbo unaopenda uwe Bora mwaka 2009 kwa kuandika namba ya mwenye wimbo na kisha tuma kwenda 15788.