Saturday, June 25, 2011

KAMATI YA BUNGE YATEMBELEA BO YA MIKOPO

Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii yatembelea HESLB PDF Print E-mail
Written by Veneranda Malima
Tuesday, 31 May 2011 17:02

Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Margaret Simwanza Sitta imetembelea Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa lengo la kupata taarifa ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya Bodi hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. George Nyatega aliwasilisha Taarifa kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa Mwaka 2010/2011 ikijumuisha malengo, mafanikio na changamoto zinazoikabili Bodi katika utekelezaji wa majukumu yake ya utoaji na urejeshwaji mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.

Kabla ya mkutano, wabunge walipata nafasi ya kutembelea ofisi za Bodi na kusalimiana na wafanyakazi katika Idara za Upangaji na Utoaji Mikopo, Fedha na Utawala, mipango, Utafiti na Teknohama, na Urejeshwaji Mikopo. Halikadhalika walisalimiana na watumishi wa vitengo vya Ukaguzi wa Ndani, Sheria na HabarĂ­, Elimu na Mawasiliano

No comments:

Post a Comment