1. NIYONZIMA AKABITHIWA NAMBA 8.
Haruna Niyonzima amesaini mkataba wa miaka 2 na yanga na kukabithiwa jezi namba 8.
mtaa: shaffih.blogspot.com
2. OKWI, MGOSI WATAKIWA VITAL.
Vital Club ya Kinshasa imewang'ang' ania washambuliaji wawili wa Simba, Mussa Hassan Mgosi na Emmanuel Okwi na wameahidi kuwasajili ingawa uongozi wa Simba hauko tayari kuwaachia.
mtaa: mwananchi
3. WAPINZANI WAMGOMBEA MGOSI.
Timu ya soka ya DC Motema Pembe na Vital zote za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), zimetangaza kumhitaji mshambuliaji Mussa Hassan 'Mgosi' wa Simba ya Dar es Salaam.
mtaa: habari leo
4. MTIBWA: KADO MALI YA YANGA.
Mtibwa sugar wamalizana na yanga na kusema sasa Shaban Kado ni mali ya Yanga. Mtibwa wako katika mazungumzo na makipa Deogratius Mushi 'Dida' na Jackson Chove.
mtaa: mwanaspoti
5. OKWI KUJIUNGA KAIZER CHIEF.
Mchezaji wa Simba Emanuel Okwi amefuzu majaribio aliyo yafanya Kaizer Chief na hivyo kutarajiawa kufanyiwa vipimo mwishoni mwa mwezi huu.
mtaa: mwanaspoti
6. APR WAKANUSHA NIYONZIMA KUJIUNGA NA YANGA.
APR wasema Haruna Niyonzima anaendelea kuitumikia APR. “Hakuna kitu katika madai hayo, Haruna ni mchezaji wa APR na anafanya mazoezi kama kawaida kujiandaa na fainali za Kombe la Peace, hajawahi kwenda Tanzania kufanya mazungumzo na Yanga au Simba,” alisema Adolph Kalisa katibu mkuu wa APR.
mtaa: habari leo
7. WYDAD & MOTEMA WAMPATIA KASEJA MKATABA.
Juma Kaseja aongezewa mkataba na simba baada ya kiwango kizuri alicho kionyesha dhidi ya Wydad na Motema. Na kufuta ndoto za yanga za kumnasa.
mtaa: mwananchi
video za majuu
No comments:
Post a Comment