Saturday, June 25, 2011
Mapunda kumvuta Mwaikimba Kenya
Kipa huyo wa African Lyon, alimwaga wino wiki iliyopita kwa ushawishi mkubwa wa kocha wa makipa wa Bandari inayoshiriki Ligi Kuu Kenya, Razack Siwa, ambaye aliwahi pia kuwa kocha wa makipa wa Yanga.
Ivo, ambaye amebeba matumaini ya timu hiyo iliyoko hatarini kushuka daraja aliiambia Mwanaspoti kuwa; "Nimeshamalizana nao na wiki mbili zijazo nitajiunga nao kwa ajili ya mazoezi kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Kenya, nimekaa kwa muda nimejifunza mazingira ya timu kila kitu kitakwenda sawa."
"Nimewashawishi pia wamsajili Mwaikimba kwa kuwa nimeona anawafaa kwa staili yao ya uchezaji na nadhani muda wowote kuanzia sasa watamsajili, hata kocha amemkubali. "Mwaikimba atasaidia sana kuwachangamsha wale vijana." Kocha wa Bandari, Rishad Shedu alisisitiza kuwa watamchukua Mwaikimba kwa kuwa ana uzoefu wa kucheka na nyavu huku kila mmoja akimuona kama mfalme na mtu aliyebeba matumaini ya Bandari.
No comments:
Post a Comment